Home Uncategorized PAUL MAKONDA AFUNGUKA MAKUNDI YANAYOTAKA KUMUANGAMIZA

PAUL MAKONDA AFUNGUKA MAKUNDI YANAYOTAKA KUMUANGAMIZA

67
0

Aliyewahi kuwa mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amefunguka kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwa anafahamu makundi yanayotaka kumuangamiza.
“Nafahamu kuna mkakati unaoratibiwa na Makundi 5 kuangamiza maisha yangu.

1) WAUZA MADAWA YA KULEVYA
2)WANUFAIKA NA MADAWA YA KULEVYA
3) MASHOGA
4)WANAOKESHA USIKU KUCHA KUTAFUTA KULIPA KISASI KWA WASAIDIZI WA DR MAGUFULI.
5) WALIOWAHI KUWA SEHEMU YA ……. Nafahamu pia juu ya mbinu zinazoandaliwa ili kuniuwa kwa faida ya familia zao pamoja na kutengeneza mashaidi wa uongo ili mnipe kesi ya uhujumu uchumi.

Mambo mawili najiuliza
1)PAMOJA NA KAZI ZOTE NZURI NILIZOZIFANYA KWA CHAMA CHANGU,SERIKALI YANGU NA WANANCHI WA DAR HAYA NDIYO MALIPO YAKE?
2)Hakika ukiwa mtumishi mwaminifu unaetetea haki za wanyonge tena ukitokea kwenye familia masikini haya ndiyo malipo yake ?

MTU aliejemga hospital , aliejenga ofc cha CCM, Magari ya police 👮‍♀️, ofc za Walimu, vituo vya police, shule za secondary mpaka na msingi, kutibu wagonjwa mpaka Meli kuja Tanzania,kuhudumia Makundi mbali mbali mpaka kuiunganisha Serikali na Viongozi wa Dini. leo hii naonekana eti natakiwa kunyongwa.

Pamoja na kwamba lipo kundi kwenye mitandao linalolipwa ili kuwaanda watanzania pale watakapo nikamata ionekane ni sawa. Hakika ipo siku Walemavu, yatima, wajane na waliotamani watoto WAO wasife kwa MADAWA ya KULEVYA SAUTI ZAO ZITASIKIKA.

Ukiona maji yametulia jua kina nikilefu.” Ameandika Makonda.

spinupdates

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here