Home Documentary KP AENDELEA KUPOKEA PONGEZI KWA KUTENGENEZA GARI LA KWANZA LA UMEME ...

KP AENDELEA KUPOKEA PONGEZI KWA KUTENGENEZA GARI LA KWANZA LA UMEME KUTENGENEZWA NCHINI KP A72.

107
0

Mtangazaji na mwanahabari maarufu nchini Masoud Ally Masoud(kipanya) ameendelea kupongezwa na watu kwa kuonyesha uthubutu wake na kuweza kutengeneza gari KP A72 gari ilo la kwanza la umeme kutengenezwa nchini na kampuni ya Kitanzania anayoisimamia ya Kay Pee Motors limewekwa kwa muda wa siku tatu Mlimani City,Dar es salaam ili kuwapa Fursa watu kuliona.

Gari(KP A72) likiwa kwenye maonyesho Mlimani City

Masoud Kipanya ameeleza safari yake ya kutengeneza gari ilo katika kpindi cha Power Breakfast

“Toka 2013 nina ndoto ya kutengeneza gari na miaka yote nilikuwa naijenga na kuibomoa na ilifika wakati nikawa nataka kiwanda kiwe Bagamoyo na nikapata sehemu nikajenga na ilivyokamilika nyumba nikagundua hii ni nyumba ya kuishi zaidi hapatoshi,Mwaka 2019 nilikutana na Mr Maganga kutoka Sido na akanipa maelezo nikaandika barua ya kutaka eneo na nikapata eneo kama ningekuwa nimelipata kwa mtu binafsi basi ningekuwa nimelipa hela nyingi sana hivyo nilivyopata eneo baada ya kumaliza kulikarabati Corona ikawa imeingia ikabidi niache kwanza ipite ndiyo nirudi tena kuanza kupambania ndoto yangu”

Masoud Kipanya akiwa na mtoto wake Salha(13) ambaye ni mkurugenzi msaidizi wa Kyeep Motors

“Baada ya kuwa na wazo tayari nikatafuta mtu wa Welding na katika kuanza kutengeneza gari sikuwa na hela yote cash hapana na toka naanza mpaka namaliza sina sehemu niliyokopa, kwa miaka miwili nilikuwa na wafanyakazi saba ambao ujanja niliyokuwa nautumia na nilisema hata wakati wa uzinduzi niliwaambia sitawalipa kwa mwezi bali nitawalipa kwa siku ili gharama zisiwe kubwa hujaja sikulipi kwa siku nilikuwa nalipa wastani wa mishahara elfu sabini mpaka laki moja, kuna vifaa vya kununuliwa, kodi hivyo wastani kwa mwezi nilikuwa natumia million tatu mpaka nne sasa hapo piga kwa miaka miwili hivyo sikukopa na wala sikuwa na ma-billion ya hela.Vitu vichache tuliagiza nje ya nchi kama Motor, Battery na Control hivyo vitu ndiyo tuliagiza nje vingine tumenunua hapa” ameeleza Masoud

Timu iliyoshirikiana na Masoud Kipanya kukamilisha utengenezaji wa Gari.

Hata hivyo wadau wa maendeleo wameendelea kumpongeza Masoud Kipanya kwa hatua hiyo aliyoifikia na kuwaaminisha watanzania kuwa wanaweza kutengeneza chochote.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here