Home Documentary UONEVU/UNYANYASAJI KUPITIA MITANDAO YA KIJAMII.

UONEVU/UNYANYASAJI KUPITIA MITANDAO YA KIJAMII.

109
0

Uwepo wa Mitandao ya kijamii umekua na faida kubwa Kwa watumiaji hususana Kwa wafanyabiashara wa mitandaoni,wanasiasa,wasanii na kuwa sehemu ya watu kutoa maoni Yao,hata hivyo kila chenye faida kina hasara zake.

Uonevu kwenye mitandao ya kijamii(Cyber bullying) ni Uonevu unaofanyika Kwa kutumia teknolojia za kidigitali Uonevu huo unaweza kufanyika katika mitandao ya kijamii(Instagram, Facebook, Twitter, Websites) na kwenye majukwaa ya ujumbe (Messaging platforms),Majukwaa ya michezo (gaming platforms) na katika Simu za mikononi .Tabia hii ufanywa Kwa lengo la kutishia ,kukasirisha au kuwa aibisha wanaokusudiwa mfano wa Uonevu ambao unatokea kwenye mitandao ya kijamii ni pamoja na Kusambaza uongo kuhusu mtu fulani,kupandisha picha au video za aibu katika mitandao ya kijamii bila lidhaa ya Muhusika.,Kutuma jumbe zenye kuumiza,matusi au kutishia katika Majukwaa ya ujumbe.na watu kutumia majina ya watu wengine nakutumia jumbe zisizo za kistaarabu Kwa niaba yao(fake account).

Nchini Tanzania watumiaji wa Mitandao ya kijamii wamekua wakikumbana na Uonevu kwenye mitandao ya kijamii hususani wanawake Kwa picha na video zao za aibu kuwekwa kwenye mitandao ya kijamii bila lidhaa Yao,hata hivyo wananchi hawana elimu ya kutosha juu ya Uonevu wa Mitandao ya kijamii na kuichukulia Kama hali ya kawaida,Wasanii kutoka nchini pia wanapitia Uonevu wa Mitandao ya kijamii Kwa watu kuwazushia taarifa za uongo,vifo au kurasa kufunguliwa Kwa kutumia majina Yao na kuwadhuluma wananchi huku wakijifanya wao ndio wasanii husika( fake accounts) mfano wa wasanii ambao wamewahi kulalamika ni Irene Uwoya,Wema sepetu,Nandy,Ommy Dimpoz,Ali kiba,Millard Ayo na wengine wengi.Neema Mkwaju ni mtumiaji wa mitandao ya kijamii na hapa anaeleza alivyonusurika kutapeliwa na mtu aliyefungua ukurasa wa Facebook na kujiita jina la msanii wa bongo fleva Nandy.”Kiukweli swala la Uonevu kwenye mitandao lipo Sana Mimi niliwahi kuambiwa na mtu alikua na account Facebook anajiita Nandy,nikajua ni Nandy kweli akasema anahitaji wafanyakazi wa Supermarket nikamtafuta akanambia nitume elfu 20 ya kuchukua form ili niweze kupata kazi hiyo,hapo nikashtuka kidogo Ila nina marafiki zangu wawili walituma na walitapeliwa wakaanza kumchukia Nandy kumbe sio yeye masikini.” Ameeleza Neema.John Mdemu mtumiaji wa mtandao wa tweeter anasema unyanyasaji wa kwenye mitandao unatokana na watu wenyewe kuweka maisha Yao wazi.”Mi nadhani Cyber bullying(Uonevu wa Mitandao) ni zawadi Kwa wote wanaofanya maisha Yao binafsi kuwa ya kitaifa Kwa mfano angalia maisha ya watu maarufu walioamua kuweka kila kitu Chao wazi ndio wanaopata Uonevu kwasababu wameshaionyesha dunia udhaifu wao lakini Kwa ambao wanaweka maisha Yao sirini bila kuweka kila kitu Chao mtandaoni haeakumbani na huo Uonevu” Anaeleza John ,Kwa uapnde wake Salma Mwanafumzi kutoka chuo cha uandishi wa Habari SJMC Anaeleza kuwa kunyanyaswa kwenye mitandao ni kawaida tu watu hawachukiliwi hatua zozote. “Imekua kama kawaida sasa watu wanatukana mitandaoni tena Kwa kupost picha yako kabisa lakini hakuna hatua wanazochukuliwa ndio maana Mimi ikinitokea uwa naona Bora niachane nae Tu na kumuona huyo mtu kama mjinga” Anasema Salma.

Cyberbullying concept. Online harassment with unfriendly mean messages. Social network violence. Internet abuse. } vector illustration

Hata hivyo nimefanya mazungumzo Mwanasaikolojia Moses Mkemwa anaeleza kuwa ni mara chache amekutana na visa vya watu wanaopitia Uonevu kwenye mitandao ya kijamii Kwa sababu jamii bado inaona masuala hayo kuwa ni ya kawaida pia ameishauri jamii kuwa makini na mitandao ya kijamii ili kuepukana na Uonevu.” Watu wanatakiwa Kuwa makini kwenye vigezo na masharti ambavyo vinatolewa katika documents mbalimbali za mitandaoni. Kumekuwa na kawaida ya watu kubonyeza Yes na I accept bila kusoma kwa makini ni mambo gani yaliyoandikwa katika document hususan kwa masuala ya privacy setting. Hii huwafanya wakubali kuweka hadharani masala yao binafsi na yakaweza kutumiwa na watu wenye malengo yenye matokeo mabaya kwao.Watu wawe makini kwa picha wanazopost mitandaoni (Za kwao au watoto wao) Wajue kwamba kuna wataalamu wa ku edit picha – Ukizingatia na tatizo la ajira lililopo kwa sasa ndiyo kabisaa.Watu wanatumia fursa kuchafua watu ili wapate pesa,Hata hivyo watoto hawana maamuzi ya picha gani zipostiwe kwa sasa lakini hapo baadae huweza kuwadhalilisha kwa sababu huwezi kujua mtu atakuwa nani hapo baadae. Kwani Teknolojia haisahau matukio!”Mwanasaikolojia Moses.

Aidha Sheria dhidi ya unyanyasaji, haswa juu ya uonevu wa mtandaoni, ni mpya na bado hazipo kila mahali. Hii ndiyo sababu nchi nyingi hutegemea sheria zingine zinazofaa, kama vile dhidi ya unyanyasaji, kuadhibu wanyanyasaji wa mtandao.Katika baadhi ya nchi zenye sheria hizi, waathiriwa wa unyanyasaji wa mtandaoni wanaweza kutafuta ulinzi, kuzuia mawasiliano kutoka kwa mtu maalum na kuzuia matumizi ya vifaa vya kielektroniki vinavyotumiwa na mtu huyo kwa uonevu wa mtandaoni, kwa muda au kwa kudumu.Hata hivyo, ni muhimu kukumbuka kuwa adhabu si mara zote njia bora zaidi ya kubadili tabia ya waonevu. Mara nyingi ni bora kuzingatia kurekebisha madhara na kurekebishaKila mtandao wa kijamii hutoa zana tofauti zinazokuruhusu kuweka vikwazo kuhusu nani anayeweza kutoa maoni au kutazama machapisho yako au anayeweza kuunganishwa kama rafiki, na kuripoti visa vya uchokozi. Nyezo nyingi kati ya hizo zinahusisha hatua rahisi za kuzuia, kunyamazisha au kuripoti unyanyasaji wa mtandaoni.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here