Home Breaking news GOOGLE WAWEKA VIKWAZO KWA URUSI

GOOGLE WAWEKA VIKWAZO KWA URUSI

140
0

Kufuatia Mgogoro unaoendelea kati ya Nchi ya UKRAINE NA RUSSIA(URUSI) Kampuni ya Google imetangaza kwamba haitaruhusu tena vyombo vya habari vya serikali ya Urusi kuonyesha matangazo, kufuatia uamuzi kama huo uliofanywa Jumamosi na kampuni mwenza ya video ya YouTube.

“Ili kukabiliana na vita nchini Ukraine tunasitisha upatikanaji wa mapato wa Google kwa vyombo vya habari vinavyofadhiliwa na serikali ya Urusi kwenye mifumo yetu yote. Tunafuatilia kwa makini matukio mapya na tutachukua hatua zaidi ikihitajika.” Google ilisema katika taarifa.

Tangazo hilo linakuja baada ya tangazo la hivi karibuni kwa vyombo vya habari vinavyohusishwa na Urusi huku kukiwa na wimbi la ukosoaji ulioelekezwa kwa majukwaa ya Big Tech katika wiki iliyopita kwa kuruhusu upataji wa mapato kuendelea licha ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Siku ya Ijumaa mtandao wa Meta (Facebook) ulisema utasitisha uwezo wa vyombo vya habari vya serikali ya Urusi kuendesha matangazo na kujipatia mapato kwenye majukwaa yake.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here