Home Breaking news RAIS SAMIA:KUTUKUZWA SI TABIA YANGU

RAIS SAMIA:KUTUKUZWA SI TABIA YANGU

108
0

“Baba Askofu umeniasa mambo ya kukataa kutukuzwa na mimi nataka nikuahidi kwamba hiyo si tabia yangu, ninajitahidi kujishusha niwe sawa na wengine, maana utumishi huu kama mipango ya Mungu ilivyo ameniweka hapa niwatumikie,Nitajitahidi na Mungu anisaidie kuwa na hekima na uvumilivu na niwe na sikio la kusikiliza yale yanayosemwa na wengine,”

Hayo yameelezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia viongozi mbalimbali wa dini katika Sherehe za kumpongeza Askofu wa Jimbo Katoliki la Rulenge Ngara, Severine Niwemugizi katika Jubilee ya Miaka 25 ya Utumishi wake wa Uaskofu leo tarehe 22 Februari, 2022 katika viwanja vya Posta Ngara mkoani Kagera.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here