Home Breaking news AKAMATWA KWA KUOA WAKE 17,BILA WAO KUJUA.

AKAMATWA KWA KUOA WAKE 17,BILA WAO KUJUA.

110
0

Polisi katika jimbo la Bhubaneshwar nchini India wamemkamata mwanaume anayedaiwa kuwalaghai wanawake 17 kwa kujifanya daktari na wakati mwingine hata afisa mkuu wa afya.
Ramesh Chandra Swain, mwenye umri wa miaka 66, alikamatwa Jumapili usiku katika nyumba moja eneo la Khandagiri huko Bhubaneswar.
Remesh anatuhumiwa kuoa kwa njia ya ulaghai wanawake 17 kutoka majimbo nane na kuwaibia pesa.
Mkuu wa polisi wa jimbo hilo, Bhubaneshwar, aliiambia BBC kwamba huenda mwanaume huyo aliwalaghai wanawake wengine kando na wanawake hao 17. “Tumepokea taarifa kuhusu wanawake watatu kati ya 17 baada ya kukamatwa kwa Ramesh.

Maafisa pia wanachunguza simu ya mkononi ya Remesh ili kujua kuhusu fedha zake

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here