Home Breaking news TAKRIBAN 100 WAFARIKI KWENYE MAPOROMOKO BRAZIL.

TAKRIBAN 100 WAFARIKI KWENYE MAPOROMOKO BRAZIL.

143
0

Takriban watu 100 wamefariki kutokana na maporomoko ya ardhi na mafuriko katika mji wa PetrĂ³polis nchini Brazil, maafisa wanasema.

Jiji hilo, ambalo liko kwenye milima kaskazini mwa Rio de Janeiro, lilikumbwa na mvua kubwa.Nyumba katika vitongoji vya milimani ziliharibiwa na magari kusombwa na maji huku mafuriko yakipita katika mitaa ya jiji hilo.

Timu za utafutaji na uokoaji zinakabiliana na tope kutafuta walionusurika.

Jeshi la Ulinzi la Kitaifa la Brazil lilisema kwenye Twitter watu 24 wameokolewa wakiwa hai hadi sasa, na vifo 94 vilivyothibitishwa.

Video zilizoshirikiwa kwenye mitandao ya kijamii zilionyesha uharibifu mkubwa na magari yakielea mitaani.

“Hali inakaribiana na kama vita… Magari yanayoninginia kwenye nguzo, magari yamepinduka, matope mengi na maji bado yapo,” Gavana wa Rio de Janeiro Claudio Castro aliwaambia waandishi wa habari.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here