Home Documentary AFUNGWA JELA KWA KUFANANA NA MHALIFU.

AFUNGWA JELA KWA KUFANANA NA MHALIFU.

136
0

Shane Lee Brown mwenye umri wa miaka 25 Kijana mweusi kutoka Nevada nchini Marekani ametumikia kifungo cha miaka sita gerezani baada ya polisi kumfananisha kimakosa na mshukiwa mzungu mwenye jina sawa na lake ambaye ana umri mkubwa mara mbili ya umri wake.

Kijana huyu alikamatwa mwezi Januari 2020 barabarani baada ya kushindwa kuonyesha kibali cha kuendesha gari (licence). Polisi wa Las Vegas walipata kibali kilichoandikwa kwa jina lake.Lakini kibali hicho kilikuwa ni kwaajili ya Shane Neal Brown halisi, mwanaume wa makamo mzungu mwenye ndevu, yalidai mashitaka ya kesi iliyofunguliwa kuhusiana na tukio hilo.

Hata hivyo Kijana huyo hakushitakiwa kwa uhalifu na sasa amewasilisha kesi ya uharibifu uliosababishwa na kufungwa kwake bila kosa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here