Home Breaking news ADAIWA KUMUUA MKEWE MJAMZITO NA KUMCHOMA MOTO.

ADAIWA KUMUUA MKEWE MJAMZITO NA KUMCHOMA MOTO.

117
0

Subira Kibona mkazi wa kijiji cha Ilanga kata ya Mlale wilayani Ileje mkoani Songwe amefariki dunia baada ya kuchomwa na kitu chenye ncha kali mgongoni kisha mwili wake kuchomwa moto na mabaki ya mwili huo kuptupwa kwenye korongo.Kitendo hicho kinadaiwa kufanywa na Mumewe Shukrani Kamwela .

Kamada wa Jeshi la Polisi mkoani humo ASP Janeth Magomi amesema walipokea taarifa za tukio hilo juu ya mwanamke huyo ambaye alipotea nyumbani tangu Januari 13 mwaka huu,ASP Magomi amesema baada ya kutoonekana kwa marehemu huyo wananchi walifanya juhudi za kumtafuta ndipo walipokuta mwili wake ukiwa umetupwa katika korongo lililopo katika moja ya pori mkoani humo huku ukiwa umechomwa na kitu chenye ncha kali maeneo ya mgongoni na kuchomwa moto.chanzo cha tukio hilo bado hakijajulikana na jeshi la polisi linaendelea kuchunguza na tayari linamshikilia mtuhumiwa.

Diwani wa kata hiyo, Yotamu Ndile, amesema tukio hilo limetokea Januari 13, mwaka huu saa 12 asubuhi baada ya mume wa marehemu kumwambia mke wake waende kwa Mganga wa kienyeji kutafuta dawa ya tumbo maarufu kama kata kamba kwani marehemu alikuwa na ujauzito wa miezi saba.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here