Home Breaking news “CHANZO CHA MOTO KARUME NI MATEJA.”

“CHANZO CHA MOTO KARUME NI MATEJA.”

258
0

Thomas Benedicto, Mfanyabiashara na Shuhuda wa moto wa Soko la Karume amezungumza kuwa chanzo cha kuungua soko la Karume ni uzembe wa mateja kwani moto ulianzia kwenye banda ambalo linadaiwa kuwa la mateja ambalo mara nyingi Mateja utumia mishumaa kuwasha mihadarati.

“Nakumbuka wakati moto unaanza mimi nilikuwepo bado sokoni sababu mimi ni moja kati ya walinzi wa siku hiyo nakumbuka sikua mbali na banda lililoanza kuungua hivyo niliitwa na kwenda kujishuhudia na kuanza kupambana kuuzima moto na nakumbuka ilibidi tukate bomba la choo cha Halmashauri na kuchukua ndoo za choo hicho ili kuweza kuuzima moto japo baadae ulituzidi nguvu. Chanzo cha moto ni mateja ambao tupo nao sokoni Karume ambao wao wanajihusisha na kuuza viatu, unajua pale sokoni kuna moja ya banda ambalo wao huwa wanalitumia kutengeneza mihadarati yao ambayo huwa wanatumia mishumaa kuitengeneza na siku hiyo mshumaa ulianguka na kuanza kuungua” ameeleza Thomas Benedicto, Mfanyabiashara na Shuhuda wa moto soko la Karume kwenye kipindi cha Power Breakfast ndani ya Clouds FM

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here