Home Breaking news RAIS ALIYEPINDULIWA MALI AFARIKI.

RAIS ALIYEPINDULIWA MALI AFARIKI.

288
0

Nchini Mali Rais aliyeondolea madarakani Ibrahim Boubacar Keita amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Jumatatu, Januari 17, 2022 akiwa na umri wa miaka 76, Familia yake wamethibitisha kifo hicho na kusema Keita amefariki majira ya saa 600 usiku kwa saa za Afrika Mashariki nyumbani kwake mjini Bamako.

Hata hivyo Keita aliiongoza Mali kwa miaka saba kuanzia mwaka 2013 hadi mwaka 2020, wakati alipopinduliwa kufuatia maandamano makubwa dhidi ya serikali kutokana na jinsi alivyolishughulikia suala la Wanajihad.Itakumbukwa kuwa, Miaka miwili iliopita, Keita aliugua kiharusi lakini chanzo cha kifo chake hakijawekwa wazi mpaka sasa

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here