Home Documentary AFISA POLISI ALIYEMPIGA RISASI 6 MPENZI WAKE AKUTWA AMEFARIKI.

AFISA POLISI ALIYEMPIGA RISASI 6 MPENZI WAKE AKUTWA AMEFARIKI.

207
0

Nchini Kemya Afisa mmoja nchini Kenya aliyetambulika kwa jina la kostabo David Nyamweka amekutwa amefariki baada ya kumpiga risasi 6 mpenzi wake Everlyn Njoki,Hata hivyo kwa sasa Everlyn anasema atakua sawa na kuishi kwa amani baada ya kusikia mpenzi wake huyo wa zamani amefariki dunia.

Mwili wa Nyamweya ulipatikana katika mto Kathita, baada ya polisi kumkagua wakakuta barua ya kufukuzwa kazi kwenye mfuko wa nguo zake.Na Barua hiyo ilisomeka kuwa alikuwa amefutwa kazi kutokana na matumizi mabaya ya silaha aliyokuwa amekabidhiwa na serikali. Njoki aliambia gazeti la Nation kuwa Nyamweya alikuwa amejaribu kumpigia simu kabla ya mwili wake kupatikana.Njoki aliambia Nation amekuwa Pwani akijificha kutokana na vitisho vya Nyamweya ambaye amekuwa akitaka warudiane.

Nyamweya aligonga vichwa vya habari Agosti 2020 baada ya kummiminia risasi Njoki katika mgahawa wa kituo cha polisi cha Laare Meru baada ya Mahusiano yao kuwa kwenye matatizo. Hata hivyo, Njoki alikuwa na Bahati kwani akaponea kifo na hata kumsamehe alipoondoka kutoka hospitali ya Kenyatta alipolazwa kwa siku kadhaa na madaktari kupambana kuyaokoa maisha yake.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here