Home Breaking news MCHUNGAJI AWAVUA NGUO WANAWAKE KANISANI NA KUWAOGESHA.

MCHUNGAJI AWAVUA NGUO WANAWAKE KANISANI NA KUWAOGESHA.

492
0

Mchungaji mmoja raia wa Ghana ameonekana katika video inayosambaa kwenye mtandaoni akiwambia waumini wake wajitokeze haraka “kuoga patakatifu” Baadhi ya washirika wanaonekana wakivua nguo zote na wakiingia ndani ya beseni Mchungaji huyo pia anasikika akisema kuwa licha ya kufahamu kwamba hatua hiyo itazua utata, hana budi kufanya hivyo ili kuheshimu maagizo ya roho mtakatifu,video hiyo ilionekana mubashara usiku wa mkesha wa Mwaka Mpya akiwafanyia washirika wa tendo ilo.

Hata hivyo nchini Nigeria Mchungaji mmoja amezindua chupi na sindiria zenye chapa ya picha yake ili kuwasaidia wanawake ambao bado hawajaolewa kuleta mvuto kwa wanaume. Mchungaji huyo aliyetambulika kwa jina la Dr J.S. Yusuf, ambaye ni mkuu wa Kanisa la Touch for Recovery Outreach International mjini Abuja, anadai kuwa aliagizwa na Mungu kuzindua chupi hizo za ‘baraka’ ili kufungua milango ya ndoa Mwaka Mpya.

Mchungaji huyo alinukuu mstari kwenye kitabu cha Hesabu 23:20 unaosema “Tazama nimepokea amri ya kubariki, naye amebariki, wala siwezi kubadili.” Pia alisema kuwa chupi hizo zinapovaliwa na wanawake, zitawasaidia kupigana na magonjwa na kupata bahati njema ya kuwavizia wanaume ambao watawaoa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here