Defao (62) amefariki Jumatatu, Disemba 27, katika Hospitali ya Laquintinie Douala nchini Cameroon, ambako alikuwa amelazwa hospitalini.Mwanamuziki huyo atakumbukwa sana kwa sauti yake nzuri na miondoko ya dansi ambayo ilivutia wengi.
Wanamuziki Ferre Gola na Fally Ipupa walikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kuwasilisha salamu zao za rambirambi, wakielezea kifo chake kuwa ni pigo kwa Afrika.