Home Documentary AMSABABISHIA KIFO MKEWE NA YEYE KUJIUA.

AMSABABISHIA KIFO MKEWE NA YEYE KUJIUA.

243
0

Steven Yamba(44) mfanyabiashara wa nchini Zambia maarufu kwa jina la Mtu Mweusi ameripotiwa kumshushia kipigo kikali mke wake wa ndoa Kangwa Mwango(33) na kufariki asubuhi ya sikukuu ya Krismas Desemba 25. Mwanaume huyo alijaribu kumpeleka mkewe  hosptali lakini alipogundua mkewe kafariki na yeye aliamua kukimbilia dukani kununua dawa ya kuulia wadudu akanywa na yeye kufariki dunia.

Watu wa karibu na familia ya Bwana Yamba wanaeleza kuwa mke huyo alikua akimlaghai mume wake kwa kujihusisha kimapenzi na Mwanaume mwingine,na baadae Mume kumfumania akiwa anafurahia tendo na mwanaume huyo na kumpelekea kupandwa na hasira na kumshushia kipigo mkewe.

Wanandoa hao Enzi za Uhai wao

Polisi nchini humo wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo na wamesema uchunguzi wa awali umeonesha mfanyabiashara huyo usiku wa saa moja katika mkesha christmas ndio alianza kumpiga mkewe hadi asubuhi na mke huyo alipoanza kuwa hoi ndio akajifanya kutaka kumpeleka hospitali ambapo alikua kafariki Dunia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here