Home Burudani NANDY:ILIKUA EXPERIENCE MBAYA AFRIMA

NANDY:ILIKUA EXPERIENCE MBAYA AFRIMA

235
0

Msanii wa Bongo Fleva anaye liwakilisha vizuri Taifa Nandy amefunguka kuwa wasanii kutoka Bongo hawakuonyeshwa ile heshima amboyo walidhani wangeipata kutoka kwa waandahaaji wa tuzo za AFRIMA ambazo walikua wanawania,na kuwafanya wavunjike Moyo hadi kutamani kuwa na Tuzo nchini Tanzania kwani wasanii wa Tanzania wanauwezo mkubwa wananguvu kwenye Mitandao ya kijamii na wanamashabiki wengi ndani na Nje ya Nchi.

Nandy ameeleza kuwa hakupendezwa na namna ambavyo waandaaji wa Tuzo hizo walivyotaka kumkatisha msanii mwenzie kutoka Tanzania Zuchu Kufanya Mazoezi kwaajili ya kutumbuiza kwenye Jukwaa la ugawaji wa Tuzo hizo ili afanye mazoezi msanii mwingine ambaye hakutaka kumtaja jina.

Hata hivyo Nandy ameongeza kuwa anashangazwa na kitendo cha baadhi ya Blogs kutoa taarifa za kuwapondea wasanii kutoka nchini hali ya kuwa hawajui wamepitia nini kwenye tuzo hizo,aidha Nandy alitarajiwa kupanda kwenye jukwaa la AFRIMA ili kutumbuiza lakini alishindwa kutokana na waandaaji kutokumpatia vitu alivyohitaji kwa aajili ya perfomance yake.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here