Home Breaking news WAZIRI WA MAJI JUMAA AWESO AJIZATITI KUONDOA KERO YA MAJI.

WAZIRI WA MAJI JUMAA AWESO AJIZATITI KUONDOA KERO YA MAJI.

310
0

Wakati Baadhi ya sehemu nchini zikiendelea kukumbwa na changamoto ya mgao wa maji,Waziri wa Maji Jumaa Aweso hajawa mbali kwani usiku wa kuamkia leo ametinga kwenye Ofisi za DAWASA kuwekea msisitizo juu ya mambo mbalimbali kwenye kipindi hiki ambacho jiji la Dar es salaam limekumbwa na mgao wa maji ambapo mojawapo ya aliyoyasisitiza ni mgao wa maji kutolewa kwa uwiano na bila upendeleo.

Kwenye kikao hicho kirefu cha mikakati kilichofanyika usiku, Waziri @Jumaa_Aweso aliongoza majadiliano ya suluhu ya muda mfupi na muda mrefu ya tatizo hili la maji pamoja na kuwapa hamasa Watumishi katika kipindi hiki kigumu na kuwataka Wataalamu watumie ubunifu na maarifa yao yote usiku na mchana kuwasaidia Wakazi wa Dar es salaam.

Jambo jingine muhimu alilolisisitiza Waziri Aweso ni kuitaka DAWASA kutoa bei elekezi kwa watoa huduma binafsi wa maji kupitia magari (bowsers) na kumalizia kwa ahadi ya ushirikiano wa Wizara katika kukabiliana na changamoto zilizopo kwa DAWASA na Bonde la Wami Ruvu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here