Mwanadada mrembo aliyepamba music video za wasanii akiwemo marehemu Albert Mangwea kwenye wimbo wa She got gwan,na Kimugine ya Linex Sunday Mjeda na kuendelea kupata umaarufu mkubwa baada ya kutoka kimapenzi na msanii wa bongo fleva Juma Jux kama mnakumbuka vizuri ile ngoma ya Jux nitasubiri aliambiwa yeye kwasababu alipata matatizo na kuwekwa kifungoni huko nchini China,Mwanadada huyu ambaye alifungwa mwaka 2013 ameachiwa rasmi na kurudi uraiani kwa kasi mpya na ukurasa wake mpya wa instagram anatumia jina la @ms.jackiecliff

Inadaiwa kuwa sakata la mrembo huyu lilianza baada ya kunaswa kwenye Kisiwa cha Macau nchini China Desemba 19, mwaka 2013 akiwa na madawa ya kulevya aina ya heroin yenye uzito wa kilo 1.1. Taarifa halisi zinaonesha kuwa Jack aliingia rasmi kifungoni Agosti 11, 2014.

Kwataarifa kamili tazama hapa.