Home Breaking news 725 WAMEFARIKI KWA CORONA NCHINI

725 WAMEFARIKI KWA CORONA NCHINI

268
0

Naibu Waziri wa Afya Dk Godwin Mollel ameeleza kuwa Watanzania 725 wamefariki kwa ugonjwa wa CORONA (Uviko-19) tangu ulipoingia nchini mapema mwaka 2020 watu hao ni kati ya 26164 walikutwa na gonjwa uo na kati yao watu 25,330 walipona.

Dkt.Mollel ametoa takwimu hizo baada ya swali kutoka kwa Mbunge wa viti maalumu Halima Mdee kuuliza kuwa ni watanzania wangapi wameugua Uviko-19 tangu ulipoingia nchini na kiasi cha fedha kilichotumika katika ugonjwa huo. “Sh158 bilioni zimetumika kununua vifaa mbalimbali ikiwepo mitambo 19 ya kuzalisha hewa ya oksijeni yenye uwezo wa kuzalisha mitungi 20 hadi 300 ambapo mitambo saba ishasimikwa na mitambo 12 ipo katika hatua ya usimikaji,” amesema Naibu Waziri Mollel.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here