Taharuki ilitanda siku ya leo katika Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro KIA baada ya abiria kutangaziwa kuwa na mlipuko wa bomu kwenye Uwanja huo.
Christina Mwakatobe kaimu Mkurugenzi wa Uwanja wa uo wa Ndege ameeleza kuwa taharuki hiyo ilikua ni mpango wa kuangalia kama matukio ya aina hiyo yakitokea nini kitafanyika,na kuongeza kuwa mpango huo ni kwa mujibu wa sheria za kimataifa za kukabiliana n na hali ya dharula katika viwanja vya ndege.