Ikiwa leo ni kikao cha kwanza cha Bunge la kumi na mbili mkutano wa
tano,Spika wa Bunge, Job Ndugai ameitaka Kamati ya Ulinzi na Usalama kuiita Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) akisema hawafanyi kazi nzuri.
amesema “Kamati ya Ulinzi Ndiyo kazi yenu kupitia hizi Kamati, waiteni kieleweke. Tumeanza nao kitambo sana”
Pia Mbunge wa Makunduchi ali hoji kwanini uzalishaji wa Vitambulisho umepungua kwa kiasi kikubwa licha ya NIDA kuomba mashine nyingine mbili za Uzalishaji.