Home Documentary MAREKANI KUILINDA TAIWAN.

MAREKANI KUILINDA TAIWAN.

324
0

Taasisi moja ya wanafikra wenye misimamo ya kulinda mpaka nchini Marekani imeeleza katika andiko lake moja la upembuzi kwamba, kuna ulazima kwa serikali ya Marekani kuweka mabomu ya atomiki katika kisiwa cha Taiwan ili kukisaidia kisiwa hicho dhidi ya China.

Taasisi ya Gatestone imeeleza katika uchambuzi wake huo kuwa, Rais Joe Biden wa Marekani anaweza kurejesha tena mkakati wa kuzuia hujuma za mashambulio kwa kupendekeza mkataba wa ulinzi baina ya Washington na Taiwan.

Sehemu nyingine ya uchambuzi huo wa Gatestone imeeleza kuwa, ikiwa yeye Biden hataki kufanya hivyo, itapasa aanzishe vituo maalumu vya silaha za atomiki ndani ya Taiwan au kuhamishia silaha hizo katika kisiwa hicho ili kiweze kujilinda.

Kwa mujibu wa taasisi hiyo yenye misimamo ya kufurutu ada, baada ya kutekwa mji mkuu wa Afghanistan Kabul, Taiwan sasa ni mtihani wa kuipima azma ya Marekani, kwa hivyo Washington inapasa ichukue hatua zisizo za kawaida kwa ajili ya kukilinda kisiwa hicho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here