Home Tech HOTELI KUBWA AFRICA KUJENGWA ZANZIBAR

HOTELI KUBWA AFRICA KUJENGWA ZANZIBAR

382
0

Hoteli Kubwa zaidi katika bara la Afrika inatarajiwa kujengwa Zanzibar ambayo itakuwa jengo la pili refu zaidi barani Afrika. Hoteli hiyo inatarajiwa kuitwa Domino Commercial Tower ambayo itakuwa na ghorofa sabini (70) ikiwa na urefu wa mita 385.

Mradi huo ambao unatarajiwa kugharimu kiasi cha dola za kimarekani 1.3 bilioni ambayo ni zaidi za shilingi trilioni 3 fedha za kitanzania, unajengwa katika kisiwa cha Chapwani kilichopo umbali wa kilometa 15 kutoka mji mkongwe Unguja.

Hii ni baada ya kampuni mbili za AICL GROUP na CEOWLAND Management Limited kuingia mkataba na kampuni ya XCASSIA yenye utaalamu wa kusanifu na kuchora ramani za majengo makubwa kama hayo duniani kwa ajili ya kutekeleza mradi huo.

Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni ya AICL Group bwana Youssef Amour amesema kuwa lengo la mradi huo ni kuiunga mkono serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika maendeleo yake yanayolenga uchumi wa blue.

Aidha, Jengo la hoteli hiyo litakuwa refu zaidi Afrika Mashariki na Kati na la pili barani Afrika baada ya jengo la The Iconic Tower lililoko nchini Misri lenye urefu wa mita 385 na ghorofa 78.

Kwa msomaji wetu, nini maoni yako kuhusu Tanzania kupitia Zanziba kuingia katika historia ya kuwa na majengo makubwa zaidi barani Afrika?

Toa maoni yako hapa chini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here