Home Micheozo HICHELEMA KUAPISHWA KUWA RAISI ZAMBIA

HICHELEMA KUAPISHWA KUWA RAISI ZAMBIA

392
1

Kakainde Hichelema ameapishwa leo tarehe 24 Agosti kuwa Raisi wa Saba (7) wa Jamhuri ya Zambia akitokea katika chama cha United Party for National Development (UPND) chama cha upinzani huku akimbaragaza vikali mpinzani wake Edga Lungu ambae ameshindwa kutetea kiti chake.

Hakainde alisha katika kinyangányiro cha uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 12 Agosti, 2021. Katika uchaguzi huo, Hakainde alimshida mpinzani wake kwa kura zaidi ya milioni moja.

Sherehe za kuapishwa kwa Raisi Mteule Hakainde imehudhuriwa na mamia ya watu mashuhuri na viongozi mbalimbali akiwemo Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hasan.

Nchi za Kiafrika zinajifunza somo kubwa katika uchaguzi huu kwani chama tawala kimekubaliana na matokeo ya uchaguzi bila kuwepo na vurugu za aina yoyote.

Msomaji wetu, unadhani kilichotokea katika Uchaguzi Mkuu wa Zambia kinaweza kutokea katika nchi za Afrika Mashariki?

Usisite toa maoni yako hapa chini.

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here