Home Micheozo GREALISH RASMI MAN CITY

GREALISH RASMI MAN CITY

292
0

Aliyekuwa Mchezaji nyota wa Aston Villa Jack Grealish mwenye umri wa miaka 25 amekamilisha kusaini mkataba wa kujiunga na kuitumikia club ya Manchester City wa miaka 6 ambao utadumu mpaka mwaka 2027.

Nyota huyo anakuwa mchezaji wa kwanza kutoka taifa la Uingereza kuuzwa kwa hela nyingi zaidi kiasi cha Euro milioni mia moja (£100million) ambacho ni sawa na fedha za kitanzania Tshs. 273.9 bilion.

Nyota huyo amepewa jezi nambari 10 ambayo alikuwa alikuwa nayo nyota wa zamani wa timu hiyo Sergio Aguero ambaye amehamia Barcelona hivi karibuni.

Grealish akishikilia jezi nambari 10 ya Man City

“Nimefurahi sana kujiunga na club ya Manchester City. City ni timu bora kwa sasa nchini Uingereza na pia ina kocha anaechukuliwa kuwa ndio kocha bora duniani. Ndoto yangu ya kuwa sehemu ya club ya Man city hakika imetimia.” Alinukuliwa Grealish baada ya kujiunga rasmi na Man City.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here