Home Micheozo RASMI MANARA YANGA

RASMI MANARA YANGA

244
0

Aliyekuwa msemaji wa club ya Simba Haji Manara leo tarehe 24 Agosti, 2021 amejiunga rasmi na club ya Dar es Salaam Young Africans maarufu Yanga ambapo aliongea na waandishi wa habari jijini dar es Salaam.

Haji Manara alikpokuwa msemaji wa simba

Kuhama kwa haji kwenda Yanga kumezua maswali mengi kwani msemaji huyo aliwahi kunukuliwa akisema hata apewe fedha zote zilizopo Benki Kuu ya Tanzania, bado hawezi kuhamia yanga, club ambayo aliita utopolo siku za nyuma alipokuwa simba.

Baada ya kutambulishwa na uongozi wa Yanga, ameahidi kufanya kazi kwa juhudi kubwa na kuifanya yanga kuwa club bingwa Afrika Mashariki na kati. Aliahidi pia kuifanya siku ya Yanga day ambayo inatarajiwa kuadhimishwa tarehe 29 Agosti, 2021 kuwa ya tofauti sana.

Aidha, Manara alishukuru uongozi wote wa Yanga kwa kumuamini kufanya kazi pamoja bila kujali kuwa alikuwa msemaji wa simba ambayo ni mtani wake wa jadi.

Ukiwa mpenda soka, maoni yako ni yapi juu ya kadhia hii? Tuachie maoni yako hapa chini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here